Tukio
hilo lilitokea juzikati kwenye chumba kilichopo katika jengo la Chama
cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Makurumla, Magomeni-Kagera, Dar.
Awali, raia wema wa eneo hilo walituma malalamiko yao kwa OFM wakidai kwamba, Dokta Kweka amekuwa akifanya ‘mauaji’ hayo ya vichanga waziwazi, hali inayowakera kupita maelezo.
Awali, raia wema wa eneo hilo walituma malalamiko yao kwa OFM wakidai kwamba, Dokta Kweka amekuwa akifanya ‘mauaji’ hayo ya vichanga waziwazi, hali inayowakera kupita maelezo.
“Jamani
ninyi si ndiyo Oparesheni Fichua Maovu? Kwa taarifa yenu hapa
Magomeni-Kagera kwenye jengo la CCM, Tawi la Makurumla, kuna daktari
anaitwa Kweka anatoa sana mimba, hasa wake za watu, njooni mumnase.”
Baada ya kupata taarifa hiyo, OFM ilipanga mtego ambapo mmoja wa waandishi wetu wa kike alikwenda kwa Dokta Kweka na kujifanya mwanafunzi wa chuo lakini ana mimba anataka kuichoropoa.
Baada ya kupata taarifa hiyo, OFM ilipanga mtego ambapo mmoja wa waandishi wetu wa kike alikwenda kwa Dokta Kweka na kujifanya mwanafunzi wa chuo lakini ana mimba anataka kuichoropoa.
Mwandishi huyo aliingia na
paparazi wa kiume aliyejifanya ni mpenzi wake aliyempa mimba hiyo. Ndani
ya eneo la tukio walipokelewa kwa bashasha na daktari huyo ambaye
alihitaji shilingi 60,000 kama gharama za kutoa mimba japo baadaye
alikubali kushusha bei hadi shilingi 45,000.
Vifaa anavyotumia Dk. Kweka.
Baadaye daktari huyo alimchukua
mwandishi wetu bila kujua kama hakuwa na mimba wala kitambi na kumpeleka
chumba cha kuchomea sindano ambapo almanusura mpango mzima uharibike
kwa kuwa mwandishi wetu hakupaswa kuruhusu daktari huyo amchome sindano
ambayo ilisadikika kuwa ni ya ganzi.
Hata
hivyo, wakati paparazi wetu akijishauri kuhusu sindano hiyo, ndipo
Stella alifika kwenye zahanati hiyo na kuingia ndani kwa dhumuni la
kutoa mimba.
Alipofika aliingia moja kwa moja chumbani kwa daktari huyo na kuchoma sindano ya ganzi bila woga kisha akaingia chumba cha kuchoropolea.
Alipofika aliingia moja kwa moja chumbani kwa daktari huyo na kuchoma sindano ya ganzi bila woga kisha akaingia chumba cha kuchoropolea.
Vifaa vinavyotumika kuchoropoa mimba.
OFM ilipata uhakika kuwa,
mwanamke huyo ameingia chumba cha kutolea mimba, ndipo ‘wapenzi’ hao
(mapaparazi wetu) waliwasiliana na wapiga picha wetu waliokuwa chobingo
na polisi ambao walitia timu na kuwanasa.
Daktari huyo na mteja wake walipelekwa kituo cha polisi na kufunguliwa jalada la kesi namba MMP/RB/567/2013 kosa likiwa kujaribu kutoa mimba huku ikibainika kuwa zahanati hiyo ni batili kwa kuwa aliisajili kama maabara.

Naye
Katibu Mwenezi wa CCM wa tawi hilo, Hashim Kimambe alizungumza na juzi na kukiri kuwa taarifa za kunaswa kwa daktari Kweka
anazo.
Alisema:
“Hata hivyo, sisi tulikuwa mbioni kumfukuza kwa sababu alipoomba
kupanga hapa alisema anaweka duka la dawa (famasi), baadaye tukashangaa
anaziba watu wanaingia ndani.
No comments:
Post a Comment