Leo video ya muziki ya Msanii Diamond
platnumz ya wimbo wa My Number one imetoka rasmi kwenye Television na
mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema ukweli ni moja ya video nzuri
sana za muziki hapa nchini na sio siri kijana huyu wa bongofleva
amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi.
Baada ya kuisikiliza kwa makini nyimbo
hii yenye mahadhi flani ya kiafrika zaidi tulifika kwenye dakika ya 2 na
sekunde 50 (2:50) ya nyimbo hii na ndipo ukatokea “ubishi” ambao
tukaona sio mbaya tukiupeleka kwa wasomaji wetu ili kupata maoni Zaidi.
Katika sehemu hii ya mwisho ya nyimbo
hii Diamond anatamka maneno ambayo baadhi ya watu tuliokuwepo katika
mabishano hayo tunasema kuwa yanamlenga mwanadada wetu muigizaji, Wema
sepetu kama “vijembe” kwakwe, diamond anamalizia wimbo wake kwa kusema
“TUACHE TULALE” maneno amabyo kwa wale wanafuatilia habari za watu hawa
wawili yalioongewa na mpenzi wa diamond wa sasa VJ penny kwenye tukio la
wapenzi hao kumrekodi mwanadada Wema Sepetu kwenye simu alipokuwa
akimbembeleza mpenzi wake wa zamani (Diamond Platnumz) warudiane, tukio
liliotokea miezi kadhaa iliyopita.
Swali likawa, Je maneno haya yatakuwa
yanamlenga Wema??? Kama siyo kwanini Diamond ayatamke sehemu ambayo hata
haihusiani nayo kwenye wimbo???
No comments:
Post a Comment