TID vs Ali Kiba
Beef hii ilianza baada ya Ali Kiba na familia yake kumshutumu TID kuwa alikuwa amepanga njama za kumuua Ali Kiba. Tuhuma hizo zilipelekea TID kupelekwa polisi lakini alitoka baada ya kesi hiyo kuonekana haina ushahidi wa kutosha.
Mpaka sasa TID bado ana hasira na Ali Kiba na hivi karibuni kupitia Facebook alimuita ‘homo’ kutokana na kitendo chake cha kumtupia shutuma hizo. “Stupid Thing Ever Happened in Bongo Music Scene is this Homo mentioned me Trying to Kill Him while am only thinkin about this Girl…No Homo,let’s make Hits,” aliandika TID.
AY vs Hermy B
Uhusiano kati ya Hermy B na AY waliokuwa maswahiba wa muda mrefu uliingia dosari baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kuelewana katika bei mpya ya kurekodia wimbo katika studio za B’Hits.
Hermy B aliwataka AY na MwanaFA kulipia kiwango kikubwa zaidi kwa single wanazorekodi kwakuwa wao ni wasanii wakubwa kitu ambacho hawakukikubali na kuamua kuvunja uhusiano na B’Hits. Baadaye Hermy B alikuja kuandika barua mbili tofauti kuelezea jambo hilo na jinsi uhusiano wao ulivyovunjika.
AY alidai angekuja kuandika maelezo kwa upande wake lakini hata hivyo hakuandika. Miongoni mwa aliyoandika Hermy kwenye barua ya kwanza ni:
Kilichotokea ni kwamba, mwaka huu mwanzoni kabisa, A.Y aliwasiliana na mimi akiwa na mipango ya kuzindua albamu yake. Na alitaka kuzinunua zile nyimbo kutoka kwangu akiwa na mpango mpya wa kuiuza albamu kwa mpango wake binafsi pasi na mimi. Nilishindwa kuelewa nini anakifanya hasa alipoomba alipie wimbo mmoja mmoja tena kwa bei ya msanii wa kawaida anaehangaika kutoka.
Niliamua kukubali kwamba ameamua kufanya hivyo na sina nguvu ya kumzuia basi nikajaribu kupata malipo halisi ya kazi yangu. Ubishi wangu ulikua kwamba msanii mdogo hawezi kulipa bei sawa ya kurekodi na msanii mkubwa, kwani hata malipo ya msanii mkubwa na mdogo baada ya kazi yoyote iwe ya matangazo ama show huwa hayafanani. Bei niliyotaja haikua millioni kumi, ni uongo mtupu na kwa wimbo mmoja niliomba nilipwe millioni 2.
Akakubali kwa bei hiyo ya Millioni 2 japo nilihisi hakuridhika kabisa. Nilimtumia mkataba wa makubaliano yetu ambayo kweli baadae aliona kwamba bei hiyo kwake ni kubwa sana hivyo hatukusaini makubaliano. Tulibadilishana meseji kwa simu kwa muda mrefu sana na niliona biashara hii itavunja urafiki wetu.
Nilifikiria sana kwamba nyimbo hizi nimekaa nazo toka 2008 bila kuingiza chochote na maisha yanaenda pia. Sikuona sababu ya kuharibu urafiki wetu wa muda mrefu kwa mabishano haya. Kwa Ujumbe wa simu nilimueleza A.Y anakaribishwa aje achukue nyimbo zoooooote anazohitaji kwa albamu yake BURE (bila malipo).Lakini nilimuomba anisamehe sitomix zile ambazo bado hazijamixiwa, ila ampatie producer mwingine amfanyie hiyo kazi.
Mpaka naona hii makala A.Y hajaja kuchukua hizo nyimbo na ndio naelewa kua hayupo na BHits tena na wala taarifa zote hizo mbili hajawahi kunipatia. Huu ndio ukweli halisi.
Lord Eyez vs Ommy Dimpoz
Beef hii ilianza baada ya Ommy Dimpoz kupost picha za Lord Eyez kwenye mtandao wa Twitter akiwa amekamatwa kwa kile alichodai kumuibia vifaa vya gari yake. Picha hizo zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na websites/blogs.
Baadhi ya watu walimlaumu Ommy kwa kitendo hicho cha kumwanika mwanamuziki mwenzie. Baada ya kukamatwa na polisi na baadaye kutoka nje kwa dhamana wakati kesi hiyo ikiendelea, Lord Eyez alirekodi wimbo Bongo Records ambamo anasikika akimtaja Ommy Dimpoz.
Beef ya chini chini kati ya Weusi na Nikki Mbishi ilianza kitambo na ilitokana zaidi na mistari ya Nikki Mbishi aliyoindika kumdiss Bonta wa Weusi kama msanii anayebahatisha na sio conscious rapper kama anavyojiita.
Hivi karibuni Nikki wa Pili alisikika kwenye mstari wake akitupa diss ya kiaina kwa Nikki Mbishi na washkaji zake kwa kusema yeye haandika punchline bali anaandika maisha.
Irene Uwoya vs Flora Mvungi
Beef ya divas hawa Bongo Movies ilitokana na uhusiano wao na H Baba. Baada ya H Baba kuachana na Irene alianzisha uhusiano na Flora waliye naye hadi sasa.
Katika mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari Irene alisikika akimponda H Baba kuwa ni mwanaume asiyejua mapenzi. Kauli hiyo ilimkera Flora ambaye naye aliamua kuongea yake na hivyo kuanzisha beef na Irene.
Afande Sele vs 20 Percent
Maswahiba haba walijikuta wakizunguana na kutupiana maneno redioni kutokana na Afande kukerwa na kitendo cha 20 Percent kugombana na waandaji wa tuzo Zanzibar waliokuwa wamewaalika wote.
Cyril vs Ommy Dimpoz
Ilikuwa ni beef iliyodumu kwa muda mfupi baada ya uzinduzi wa documentary ya Cyril ‘From Day One’ uliokuwa umepangwa kufanyika Club Billcanas kutaka kuzuiwa na baraza la sanaa Tanzania kwa madai kuwa ni raia wa Kenya. Jambo hilo Cyril aliliona kama hujuma iliyokuwa imepangwa na Ommy aliyekuwa na show siku hiyo hiyo Maisha Club.
Chidi Benz vs Ney wa Mitego
Pamoja na kuanzisha beef kali na waigizaji wa Bongo Movies kutokana na wimbo wake Nasema Nao, Ney wa Mitego alimdiss pia King Kong Chidi Benz kwa kuamua kujitoboa pua na kuweka heleni. “Au mwenzetu shoga” alisema Ney kwenye ngoma hiyo.
Kwa upande wake Chidi Benz baada ya kuhojiwa ili aseme alivyouchukulia mstari huo na kusema hamfahamu Ney wa Mitego.
Diamond vs H Baba
Beef ya Diamond na H Baba ilitokana na wimbo ‘Nataka Kulewa’ wa Diamond. H Baba alidai kuwa Platnumz alimuibia idea hiyo wakati walipokuwa wakirekodi wimbo wenye jina kama hilo katika studio za G Records ambapo alikuwa amepanga kumshirikisha Q Chief. H Baba alionesha vielelezo vyote kuthibitisha kauli yake licha ya baadhi ya watu kudai anataka umaarufu.
Q Chief vs Adam Juma
Hii ni beef ya hivi karibuni tu ambapo Q Chief anamshutumu Adam Juma kwa kutoitoa video yake aliyomfanyia. Q analaumu kuwa Adam amemharibia mipango yake na huku akimrudisha nyuma kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment