Monday, December 31, 2012

JULIO WA BIG BROTHER AFRICA SASA KWENYE MZIKI.


Julio
Mwakilishi wa Tanzania kwenye jumba la Big Brother Africa 2012 kwa sasa ameanza kazi zake za mziki rasmi na atafanya Nyimbo na Producer tofauti wanaofahamu kipaji chake chenye miaka 11 kwa sasa.Julio ameongea na sammisago.com na kusema alikuwa na rafiki yake kutoka Angola na walienda Nigeria kufanya Reality Show ya 600 Life Style na wakati huo alikuwa tayari ameanza kufanya kazi na producer Mtanzania anaye fanya kazi zake Canada, Pia producer Ludigo na Luchi walitaka kufanya nae kazi. Fahamu kuwa kuna wimbo wa Julio unafanyiwa kazi na Luchi na Producer mwingine kutoka California. Pia Julia alisema anampango wakufanya wimbo na Mwakilishi mwenzake `Hilda'. Wimbo Mpya wa Julio Unaitwa Cheers.

No comments:

Post a Comment