Mwigizaji Dinno alikua rafiki mkubwa sana wa Marehemu Sajuki na ndio alikua analala hospitali na Sajuki pale Muhimbili.
Ameongea
Exclusive na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutoa maneno ya mwisho ambayo
aliyasikia kutoka kwa Sajuki akimzungumzia mke wake ambae ni Wastara.
Kwa
haraka haraka mwigizaji Wastara amesifiwa sana na watu mbalimbali kwa
moyo wake wa ushujaa wa ukweli wa upendo kwa Sajuki japo walipitia
matatizo makubwa na mengi kwenye maisha yao.
Masanja Mkandamizaji
na Arnold Kayanda ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopaza sauti
zao kupitia mitandao ya kijamii kumsifia Wastara kwa moyo wa upendo.
Tukirudi
kwa Dinno, namkariri akisema “tulipokuwa Arusha sisi watatu tu Sajuki
alionyesha ishara ya kukata tamaa, siku moja tulikua hotelini usiku kama
saa tisa hivi Wastara alikuja kuniamsha kwenye chumba changu nikaenda
kwa Sajuki, alikua anaumwa sana akamwambia Wastara naomba mpigie mama
niongee nae, Sajuki akamwambia mama yake mzazi kwamba Wastara nampenda
sana, kanizalia mtoto mzuri anaitwa Farhini, naomba msimsumbue naomba
msimpe shida yoyote amenisaidia sana, naomba mumwachie Farhini amlee
amtunze mtamuona, yalikua maneno mazito sana mpaka machozi yakawa
yananitoka”
Kwenye mstari mwingine Dinno amesema jambo jingine
ambalo Sajuki aliliongea mwishoni ni kuhusu upendo miongoni mwa wasanii
wa movie Tanzania, namkariri akisema “alikua ananiambia hebu jitahidi
kuwa unakaa na wasanii, unajua sisi hatupendani Dinno ila mimi iko siku
nitakuja kuropoka nikae na watu niwazungumzie tuweke upendo pamoja,
tukishapendana tutafanya kitu Dinno”
No comments:
Post a Comment