Saturday, January 19, 2013

MAIMAMU WAPINGA GESI ISITOKE MTWARA

Maelfu ya shura ya maimamu yameunga na wananchi wa mikoa ya Kusini, kuitaka Serikali isitishe mpango wa kusafirisha gesi asilia kwenda Dar es Salaam. Aidha, wametaka uwekwe mtambo wa kufua umeme uliokusudiwa hapo awali mkoani hapo.Akisoma tamko kwenye hadhara ya waumini wa Kiislam mjini hapa, Ustadhi Mohamed Salim, alisema kwa kuwa wanaamini serikali yao ni sikivu  basi isitishe zoezi zima la ujenzi wa bomba mpaka pale suluhisho la tatizo hilo litakapopatikana baina ya wananchi na viongozi.
Tamko hilo lilotolewa lilitolewa jana na Shura ya Maimam katika kongamano la dini ya waumi wa Kiislamu lililofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini hapa.


Aidha Ustadhi Salim amesema kuwa kumekuwepo na majibu  ya kutoridhisha na ya kuwakashifu wananchi wa Mtwara kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Waziri wa Madini na Rais mwenyewe, ambayo yanajaribu kueleza vitu vingine na si hoja yenyewe ya wananchi wa Mtwara.
“Majibu yanayotolewa na viongozi hao yanaonyesha na yanajikita katika kuelekea upingaji wa kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar lakini sababu ya kukataa gesi isitoke si hivyo…,” alisema.
Alisema serikali haina budi kubadilika kimawazo na kuona kuwa mikoa ya kusini ina haki ya kuendelezwa kiuchumi na kuachana na kasumba ya kila kitu kupelekwa Dar es Salaam.
“Ifike wakati sasa wa kuendeleza mikoani … mikoa mingine ili mrundikano wa watu uliopo Dar upungue…na usawa wa maendeleo kati ya mikoa mbalimbali iliyopo hapa Tanzania.
Alisema katika historia mkoa wa Mtwara umetengwa kwa muda mrefu tangu enzi ukoloni.
Akitoa mfano Imamu huyo alisema Mtwara ilikuwa na  reli ikaondolewa, bandari kwa sasa haitumiki, taa kubwa za uwanja wa ndege  zilizoondolewa na kupelekwa Arusha.
Alisema leo gesi imegundulika wanataka kuiondoa na kuifanya Mtwara ibaki kuwa maskini.
Katika tamko lao hilo walisema wamechoshwa na hali hiyo na wako tayari kufa kwa ajili ya gesi.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment