Thursday, January 3, 2013

MBOWE ACHARUKA; ASEMA SIKUMTANGAZA DR.SLAA MGOMBEA URAIS 2015



- “Nilisema sigombei, hivyo hatugombanii vyeo, tunaheshimiana na tunaelewana. Niliongeza kuwa 2010 sikugombea, tulimtuma Dk. Slaa na alitosha katika nafasi ile na hakuna anayebisha kuwa hakutosha maana alitupatia wabunge wengi.

Niliwaambia kuwa mimi ni mwenyekiti, nitasimamia kanuni na taratibu za kuwapata wagombea wazuri, tangu rais, wabunge na madiwani, na nikasema ni vema tukawatambua wagombea mapema kwani hatutakubali wale wanaojiunga mwishoni kutoka CCM kwani tumegundua ni mamuluki.

Hao wananilisha maneno kwa kunitolea kauli tofauti na niliyoisema kulingana na malengo yao,” - Mbowe!

No comments:

Post a Comment