Wednesday, January 2, 2013

"NILIBADILI WANAUME KAMA NGUO LAKINI BADO SIKUFANIKIWA, MWAKA HUU SITAKI KUPENDWA"....BABY MADAHA



MSANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha amefunguka kuwa mwaka uliopita wa 2012 aliteswa na mapenzi kiasi kwamba hakumpata mwanaume sahihi wa kuendesha naye maisha. 

Akiongelea mikakati yake mwaka huu , Baby Madaha alisema alifanikiwa katika mambo mengine lakini katika mapenzi hakufanikiwa na kumfanya abadili wapenzi na mwisho kubaki bila ya mpenzi kutokana na kushindwana kitabia na wanaume tofauti.

“Nilijitahidi sana kumpata mwanaume mwenye mapenzi ya kweli lakini sikufanikiwa, nilibaki kuumia moyo tu, hivyo mwaka huu sitaki kurudia tena ujinga huo, nimejipanga kufanya kazi zaidi na kuachana na wanaume,” alisema Baby.

No comments:

Post a Comment