Tabia mbaya! Staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’
wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya
Katika tukio hilo lililojiri juzikati
kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la
Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya
basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.
Mara baada ya kutimba uwanjani hapo
wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki
kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo
yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond
ambaye alimpachika mapajani
Shushushu wetu aliwapiga chabo
‘wakifanya yao’ hadi Diamond alipokwenda stejini na kuangusha bonge la
shoo huku akimwacha Linah mpweke.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli
mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo,
basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.
Mwanahabari wetu alipomuuliza Linah kuhusu ishu hiyo, alifunguka: “Weweee…hakuna ni mapozi tu na wala usiandike hiyo habari.”
Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah
kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo
wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsiriwa kuwa inaonekana ni katabia kao
kabaya wanakaendekeza.
SOURCE: GPL
No comments:
Post a Comment