Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel
Grayson ‘Gwantwa’ yupo hatarini kukatwa mkono kutokana na jeraha la
chupa alilolipata hivi karibuni.
Tukio la Aunt kupigwa chupa na mwanamke
aliyetajwa kwa jina moja la Yvonne nje ya Club Bilicanas, Posta jijini
Dar, lilitokea Agosti 26, mwaka huu wakati staa huyo alipokwenda
kujiachia na mshosti zake.
Baada ya kupigwa chupa siku hiyo, Aunt
alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini bahati mbaya alikosa
daktari wa kumtibu hivyo akalazimika kwenda kutibiwa katika Hospitali ya
Dk. Mvungi, Kinondoni ambapo alishonwa nyuzi sita pamoja na dawa za
kukausha kidonda.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt ni
muoga wa dawa na wakati kidonda kikiwa bado hakijapona vizuri aliacha
kumeza dawa alizopewa.
Chanzo hicho kilisema tatizo la staa
huyo kukatisha dozi lilisababisha kidonda kishindwe kupona na badala
yake kikaanza kutengeneza usaha na taratibu mkono ukaanza kuoza.
“Mkono ulifikia hatua ukaanza kuoza kwani licha ya kushonwa lakini kilibadilika rangi ndipo alirudi hospitali.
Imeelezwa kuwa mapema wiki hii, Aunt
alirudi tena katika Hospitali ya Dk. Mvungi na kusafishwa upya kidonda
baada ya madaktari kugundua tatizo lilizidi kuongezeka.
Kwa mujibu wa nesi wa hospitali hiyo
aliyeomba hifadhi ya jina lake, hali ya Aunt ilimshtua daktari,
akamwambia aombe Mungu kwani kidonda kilichimbika sana na tatizo kama
hilo huweza kusababisha mtu kukatwa mkono.
“Iligundulika mkono ulikuwa unaoza,
daktari alimwambia amuombe Mungu kwani hatua iliyokuwa imefikia ni mbaya
hivyo asipokuwa makini tatizo hilo litamfanya akatwe mkono,” alisema
nesi huyo.
Aunt alipigwa chupa akigombania penzi la mwanaume na Yvone .
-Gpl & Aman
No comments:
Post a Comment